Posts

Showing posts from April 26, 2015

REBECCA MALOPE: Malkia wa muziki wa injili Afrika ya Kusini

Image
Rebecca Malope amezaliwa mwaka 1968 karibu na Nelspruit mji mkuu wa Mpumalanga, Siku za nyuma alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu hivyo alishindwa kuendelea kusoma, kiufupi tu ni kwamba alipokuwa motto mdogo alikuwa akitumia baiskeli za walemavu kutembelea kutokana na kuumwa sana na kwa muda mrefu ambapo iliwapelekea hata madaktari kuamini kwamba hataweza kutembea tena. Malkia wa nyimbo za injili Afrika ya Kusini Rebecca Malope akiwa ameshika tuzo. Familia yake ilikuwa maskini sana, ambapo mnamo mwaka 1986 Rebeka pamoja na dada yake Cynthia walitembea umbali wa kilomita 400 kutoka nyumbani kwao kwenda   Johannesburg mjini Evaton kutafuta kazi. Mnamo mwaka 1986 Rebecca aliingia kikundi cha kusaka vipaji kilichojulikana kama ‘Shell Road Fame’ lakini hakufanikiwa.   Hakujali hilo akaingia tena mwaka uliofata na hatimae akashinda kuwa mwimbaji bora katika aina ya usololisti pamoja na Shine On . Tuzo aliyoipata baada ya kuwa mshindi iliwakilisha katika soko la muzi...

ROSE MUHANDO: Malkia wa muziki wa injili nchi Tanzania

Image
Rose mhando ni muimbaji   maarufu wa nyimbo za   injili nchini Tanzania na afrika ya mashariki kwa ujumla ambaye alianza kutambwa mwaka 2004 na albamu ya Uwe Macho ambayo ilipendwa na watu wengisana. Awali muimbaji huyu kabla ya kuwa mkristo, alikuwa muumini wa dini ya kiislamu, baadaye alipokuwa na umri wa miaka tisa anasema akiwa amelala alipata maono ya Yesu Kristo. Pia anasema aliteseka kwa muda wa miaka mitatu na kuamua kubadilisha dini kwa kupokea wokovu na kuwa mkristo, ambapo baadaye alianza kuimba muziki wa injili kama mwalimu wa kwaya inayojulikana kama kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la Anglikana linalofahamika kama Chimuli lilipo mkoani Dodoma. Tangu aanze kuimba muziki wa injili amefani kiwa kutunukiwa tuzo tatu ambapo tuzo ya kwanza alitunukiwa tuzo ya muimbaji bora wa kike na nyimbo za dini 2005 tuzo ya Tanzania Music Award wimbo ukiwa “Mteule uwe macho”, 2009 alipata tuzo ya Tanzania Gospel Singer Awards ya mwimbaji bora nchini Tanza...