EPHRAIM SEKELETI: Muimbaji machachali nchini Zambia
EphraimSekeleeti Mutalange ni muimbaji wa nyimbo za injili nchini Zambia, ambae
alianza kuimba akiwa na umri mdogo akiwa kanisani na kupata uzoefu wa kuimba
pamoja na kupiga kinanda.
![]() | |
| Ephraimu Sekeleti akiwa anaimba jukwaani |
Kadri
siku zilivyozidi kwenda akajiunga na kikundi kilichojulikana kama Virtue for Christ ambapo akiwa katika kikundi hicho aliimba kwa kipindi wa miaka miwili. Mnamo
mwaka 2002 alipata kiasi kidogo cha pesa na kwenda nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya kurekodi
lbamu yake ya kwanza.
Licha
ya kuchukua uamuzi huo wa kwenda kurekodi, lakini mambo yalikuwa tofauti na
alivyo tarajia, kwani alifanikiwa
kurekodi nyimbo mbili pekee. Akiwa anajaribu kuzoea mazingira alijiunga na
kikundi cha maigizo mjini Pritoria na kupata nafa ya kuimba mbele ya raisi.
Wakati
nafasi nyingi zilivyozidi kujitokeza zililimfanya awaze kuachana na muziki wa
injili na kuimba nyimbo za kidunia, lakini alijitahidi kuwa mwaminifu na
kuendelea na muziki wa injili.
Kadri
sikuku zilivyozidi kwenda, hatimaye mlango ukafunguka na akapata nafasi ya
kurekodi albamu yake ya kwanza iliyo julikana kama Temba Baby, pamoja na kupata
mafanikio katika albamu hii ambayo yalimpelekea ajisikie kurudi nyumbani kwao
nchini Zambia na kuwekeza pesa alizopata kwa ajili ya albamu ya pili na
kufanikiwa kuitoa ambayo ilikuwa inajilikana kama Limo Ndanaka.
Albamu
hii ya pili ilifanya vizuri kwa wakristo na kushika nafasi ya juu katika muziki
wa injili. Pia Ephraim alipata nafasi kutembelea
nchi mbalimbali kwa ajili ya uimbaji nje
ya Zambia , kama vile Namibia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Zimbabwe na
Autralia. Kijana huyu mdogo ni mfano wa waimbaji
wanaoiwakilisha nchi ya Zambia kwa kile anachokifanya.
Pamoja
na kufanya muziki nchini Zambia, lakini pia kuna albamu yake aliyoimba kwa
lugha ya kiswahili ambayo ilitafsiriwa kutoka lugha ya kizamzia, moja ya nyimbo hizo ni kama vile Uniongoze na uruma zako, Moto unawaka, Mungu usiyelala nanyingine ambazo aliirekodia nchini Tanzania.
Ephraim
sekeleti amezaliwa septemba 26, 1983 kalulushi nchini Zambia.Pia albamu alizonazo mpaka sasa ni pamoja na Temba Baby, Limo Ndanaka, Lesa Tekeleshi, Lekeni Iloke na nyinginezo.


Comments
Post a Comment