Pata kumfahamu muimbaji mahiri Solly Mahlangu.



Muimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili, ambae pia ni Mchungaji Solly Mahlangu, ni moja kati ya wimbaji maarufu kutoka nchini Afrika ya kusini, barani Afrika. Ni msanii ambae amekuwa akiimba nyimbo zake moja kwa moja akiwa jukwaani kwa kutumia na vyombo mbalimbali vya kisasa vya muziki, tofauti na tulivyo zoea kuona  wasanii wengine wakirekodi kwanza nyimbo zao studio, na baadae kutumia kanda wanapokuwa wanaimba katika majukwaa  japo kwa sasa baadhi yao wameanza kufanya kama Mahalangu.



 
Mwimbaji ambae pia ni Mchungaji Solly Mahlangu akiwa jukwaani.
     Mahalangu amekuwa akifanya muziki ambao unawavutia watu wengi sana ulimwenguni, kutokana na uimbaji wake wa kipekee pamoja na ubunifu alionao akiwa  anaibma jukwaani
Mahalangu  ni msanii ambae  amezaliwa mjini Johannesburg nchini  Afrika ya kusini 1971, amelelewa na mamayake, pia aliokoka  akiwa na umri dogogo . Ameanza utumishi wa uimbaji wa nyimbo za injili akiwa na miaka 10 ambapo maishayake yote tangu utoto amekua akiishi,  mjini Johanessesburg.

Akiwa  umri wa  miaka 18 alichukua uamuzi wa  kufunga ndoa na mke wake mpendwa Khosi Mahalangu, katika ndoa yao, pia wamejaliwa watoto watatu wa kike ambao ni Thando, Amani na Asante.
Baada ya kutumika kwa muda  wa miaka 20 katika huduma  hiyo kama kiongozi wa kuabudu na mkurugenzi wa muziki, baadaye akawa mkurugenzi wa muziki kitaifa katika Kanisa la Victory Fellowship chini ya Dk.  M.A. Maphalala .Akiwa kwenye huduma ya uimbaji, aliweza kusafiri nchi mbalimbali zilizopo barani  Afrika akiwa pia kama kiongozi wa mafunzo ya masuala ya kiroho.
.
Pia mchungaji Mahlangu  katika uimbaji wake ni mzoefu wa kurekodi muziki tangu 1991, akiwa na jumla ya albamu nne ambazo ni PRAISE HIM IN AFRICA 1970, MWAMBAMWAMBA, NGISONDELA KUWE  2014NA OBRIGADO 2010.  Hata hivyo amekuwa kiongozi wa kanisa ambalo alianzisha  linaloitwa Word Praise Christian Center International lililopo eneo la Tembiza mjini Johanesburg.






    Kanisa hilo likiwa Chini ya Mchungaji mahlangu  akisaidiana na mkewe katika uangalizi, kanisa hilo likazidi kukua na kupata umaarufu mkubwa. Miongoni mwa albamu zilizo bamba zaidi kitaifa na kimataifa ambazo ameimba moja kwa moja ‘live’ katika matamasha ya kimataifa kwa njia ya DVD na CD ni Obrigado na Mwamba Mwamba.
Pia  Mchungaji mahlangu amekuwa akifanya huduma ya uimbaji  sambamba na kuendesha kanisa jambo ambalo katika mazingira ya kawaida ni watu wachache sana wanaweza kufanya hivyo hiki ni kitu cha kuvutia zaidi
Mwaka 2002 aliibuka mshindi wa tuzo tatu za SABC Gospel Crown Awards tukio ambalo liliwashangaza wengi. Vilevile kutokana na kudhiirisha ubora wa nyimbo anazoimba, akaingia tena kwenye tuzo ya 18 ya MTN South African Music Awards.

Mahlangu pia amewahi kuingia katika shindano la kuwania tuzo ya albamu bora ya Best Traditional Faith Music na Best live DVD akishindana na wakali wenzake kama Concord Nkabinde na Simphiwe Dana.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Ambwene Mwasongwe: Msanii anaekonga mioyo ya watu

Historia ya muziki wa injili

REBECCA MALOPE: Malkia wa muziki wa injili Afrika ya Kusini