Pata kumfahamu muimbaji mahiri Solly Mahlangu.

Muimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili, ambae pia ni Mchungaji Solly Mahlangu, ni moja kati ya wimbaji maarufu kutoka nchini Afrika ya kusini, barani Afrika. Ni msanii ambae amekuwa akiimba nyimbo zake moja kwa moja akiwa jukwaani kwa kutumia na vyombo mbalimbali vya kisasa vya muziki, tofauti na tulivyo zoea kuona wasanii wengine wakirekodi kwanza nyimbo zao studio, na baadae kutumia kanda wanapokuwa wanaimba katika majukwaa japo kwa sasa baadhi yao wameanza kufanya kama Mahalangu. Mwimbaji ambae pia ni Mchungaji Solly Mahlangu akiwa jukwaani . Mahalangu amekuwa akifanya muziki ambao unawavutia watu wengi sana ulimwenguni, kutokana na uimbaji wake wa kipekee pamoja na ubunifu alionao akiwa anaibma jukwaani Mahalangu ni msanii ambae amezaliwa mjini Johannesburg nchini Afrika ya kusini 1971, amelelewa na mamayake, pia aliokoka akiwa na umri dogogo . Ameanza utumishi wa uimbaji wa nyimb...