Posts

Showing posts from April 20, 2015

Ambwene Mwasongwe: Msanii anaekonga mioyo ya watu

Image
Ambwene Mwasongwe ni msanii ambae nyimbo zake zimebeba ujumbe murua,   ambao unawavutia watu wa aina mbalimbali walio wakristo na hatata watu wa dini zingine   kusikiliza. Mwasongwe amekuwa na uimbaji wa tofauti na wasanii wengine Afrika ya mashariki na barani Afrika , hasa katika utunzi wa nyimbo zake ambazo zinakuwa zimebeba ujumbe mzito ambao mtu yeyote akisikiliza zinamfanya atafakari zaidi. Ambwene Mwasonwe akiwa anaimba. Moja kati ya nyimbo zake ambazo watu wengi wamekuwa wakipenda kusikiliza ni MAJARIBU NI MTAJI, MISULI YA IMANI na UPENDO WAKWELI hizi ni baadhi ya nyimbo za Mwasongwe   ambazo   zinasikilizwa kwa kiasi kikubwa. Msanii huyu amezaliwa mwaka 1985, ambapo alianza kuimba nyimbo za injili akiwa na umri wa miaka 16 na kutoa albamu yake ya kwanza inyoitwa Majaribu ni mtaji , akiwa na miaka 19, ikiwa mpaka sasa ametoa albamu tatu yapili ikiitwa Heshima ya mrefu ni mfupi maarufu kama mzee wa siku, na ya tatu ni Misuli ya imani. ...