EPHRAIM SEKELETI: Muimbaji machachali nchini Zambia

EphraimSekeleeti Mutalange ni muimbaji wa nyimbo za injili nchini Zambia, ambae alianza kuimba akiwa na umri mdogo akiwa kanisani na kupata uzoefu wa kuimba pamoja na kupiga kinanda. Ephraimu Sekeleti akiwa anaimba jukwaani Kadri siku zilivyozidi kwenda akajiunga na kikundi kilichojulikana kama Virtue for Christ ambapo akiwa katika kikundi hicho aliimba kwa kipindi wa miaka miwili. Mnamo mwaka 2002 alipata kiasi kidogo cha pesa na kwenda nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya kurekodi lbamu yake ya kwanza. Licha ya kuchukua uamuzi huo wa kwenda kurekodi, lakini mambo yalikuwa tofauti na alivyo tarajia, kwani alifanikiwa kurekodi nyimbo mbili pekee. Akiwa anajaribu kuzoea mazingira alijiunga na kikundi cha maigizo mjini Pritoria na kupata nafa ya kuimba mbele ya raisi. Wakati nafasi nyingi zilivyozidi kujitokeza zililimfanya awaze kuachana na muziki wa injili na kuimba nyimbo za kidunia, lakini alijitahidi kuwa mwaminifu na kuende...