Historia ya muziki wa injili

Je umewahi kusikia wimbo ambao umekutoa sehemu ulipo na unataka kuwaeleza rafiki zako kuhusiana na hicho ulichokisikiliza? Vizuri hii ni aina ya hisia uliyowahi kuiskia kutoka kwenye nyimbo za injili. Kwa uhalisia, neno Injili inamaanisha habari njema. Muziki wa injili ni moja ya chombo bora  cha usafiri ambacho uaminika na wakristo katika kueneza injili kwa wasikilizaji ulimwenguni kote.
 Muziki huu  ulichipuka katika tamaduni za kitajiri katika  makanisa ya kiafrika na kimarekani kuanzia miaka ya 1800, Makanisa hayo yalioko huko   umoja wa Marekani kusini ya alianza kukusanyika katika mitindo  mbalimbali ya muziki kwenye  ibada  za kuabudu  pamoja na kusifu katika roho pamoja na nyimbo za zaburi. Aina ya muziki uliokuwa ukiimbwa awali kanisani ulikuwa ukihusisha kupiga makofi na kucheza stepu.
Moyo wa utamaduni  wa muziki wa injili ulikuwa ukitumia kwaya. Kwaya za kanisa zilikuwa zikiundwa na kundi la waimbaji ambao walikuwa wakijitolea kwa ajili ya  kuabudu  kutoka ndani ya kanisa. Ilikuwa ni rahisi kutofautisha  wanakwaya wa kikundi moja na kingine kwasababu walikuwa na kawaida ya kuvaa sare ambazo zilikuwa zakipekee.  Kwa mfano kuna maigizo ambayo yamewahi kuigizwa kama wakaka wa bluu  (Blues Brothers), matendo 2 ya dada (Sister Act 2).
Aina ya muziki uliokuwa ukiimbwa na kwaya ulifata muito na utekelezaji sambamba na kutumia tamaduni za nyimbo za zaburi
Mfumo wa utamaduni wa nyimbo za injili ulibadirika miaka ya 1930 wakati Thomas A. Dorsey alianza kazi ya kutembelea makanisa ya ubatizo ndani ya mji wa Illinois Chikago. Dorsey alikuwa mwanamziki maarufu  wa zamani ambaye alifanya kazi na wachezaji maarufu kama Ma Rainey na  Hudson Tamp Red Whitaker. Pia Dorsey alijikita zaidi katika masomo ya utamaduni wa nyimbo za mziki wa injili za huzuni na rumba. Huu ni mtindo mpya wa muziki unaojulikana kama injili ya huzuni(gospel blues), ambao ulianza zamani. Lakini pia mwishoni mwa miaka ya 1930 aina hii ya muziki ilichukua nafasi ya juu kama mfumo mpya wa utamaduni wa injili


Thomas A. Dorsey mwanamuziki wa injili wa zamani kutoka mji wa Illinois Chikago

Muziki wa injili uliendelea kukua  katika miaka ya 1930. Kulikuwa na mitindo mikuu mnne ya muziki huu ambayo ni mtindo wa kikundi cha watu  wanne ,utamaduni wa injili,njia ya injili ya kisasa,vilevile  kusifu na kuabudu .Injili ya  mtindo wa vikundi vya wanne ni moja yenye idadi ndogo ya  waimbaji wa kiume ambao wanaimba  mziki pamoja na amani .Tofauti kubwa kati ya  injili ya utamaduni na injili ya kisasa ni kwamba imeweka juhudi kubwa kwenye  uimbaji  binafsi kwenye  kikundi cha waimbaji. Waimbaji wengi wa injili ya kisasa hawapendi kuimba kwenye   kwaya. Kusifu na kuabudu  ni mtindo mchanganyiko    wa injili ya kisasa  na ya  utamaduni ,kwenye  kusifu  kiongozi  ana kikundi  kidogo kinacho saidia kwenye  mkusanyiko wa watu  kwenye  kuimba   mziki wa injili.        
Muziki wa injili umekua kwa sehemu kubwa sana ukilinganisha na zaidi ya miaka miaka miambili iliyopita, tangu kuanza kwa  muziki huu, kwani katika kipindi hiki kuna waimbaji wengi  tofauti na zamani.
Pi muziki huu umekuwa ni moja ya dhana inayotumiwa na wasanii mbalimbali ulimwenguni  katika kueneza habari njema za Yesu Kristo, kumsifu Mungu,kuabudu pia kutoa jumbe mbalimbali za maneno matakatifu ya Mungu.


Comments

Popular posts from this blog

Ambwene Mwasongwe: Msanii anaekonga mioyo ya watu

REBECCA MALOPE: Malkia wa muziki wa injili Afrika ya Kusini