REBECCA MALOPE: Malkia wa muziki wa injili Afrika ya Kusini
Rebecca Malope amezaliwa mwaka 1968 karibu na Nelspruit mji mkuu wa Mpumalanga, Siku za nyuma alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu hivyo alishindwa kuendelea kusoma, kiufupi tu ni kwamba alipokuwa motto mdogo alikuwa akitumia baiskeli za walemavu kutembelea kutokana na kuumwa sana na kwa muda mrefu ambapo iliwapelekea hata madaktari kuamini kwamba hataweza kutembea tena.
![]() |
Malkia wa nyimbo za injili Afrika ya Kusini Rebecca Malope akiwa ameshika tuzo. |
Familia yake ilikuwa maskini sana, ambapo mnamo mwaka 1986 Rebeka pamoja na dada yake Cynthia walitembea umbali wa kilomita 400 kutoka nyumbani kwao kwenda Johannesburg mjini Evaton kutafuta kazi.
Mnamo mwaka 1986 Rebecca aliingia kikundi cha kusaka vipaji kilichojulikana kama ‘Shell Road Fame’ lakini hakufanikiwa. Hakujali hilo akaingia tena mwaka uliofata na hatimae akashinda kuwa mwimbaji bora katika aina ya usololisti pamoja na Shine On.
Tuzo aliyoipata baada ya kuwa mshindi iliwakilisha katika soko la muziki, ambapo alipata sapoti wa huduma ya mtunzi wa nyimbo Sizwe Zako na mwekezaji Peter Tladi ambae alikuwa mkurugenzi wake. Ablamu ya kwanza ya muimbaji huyu ambayo ilikuwa mpya katika soko la muziki, haikuingiza mauzo ya kutosha. Baada ya hapo Rebecca aliwasha muziki wa injili na kupokelewa na vyombo vya habari ambapo vilikuwa vikipiga nyimbo zake hasa upande wa redio, hivyo vilikuwa na umuhimu kwa waimbaji wa eneo hilo.
Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya OKVT ya msanii bora wa kike Afrika ya kusini. Mwaka 1993 inakadiriwa kuwa zaidi ya wasikilizaji milioni moja walimpigia kera na kumfanya awe muimbaji bora wa tuzo ya maonyesho ya Coca Cola Full Blast Music Show, alishinda mwaka 1993 na 1994, pamoja na thamani kubwa ya kuuza albamuyake , ambapo aliuza zaidi ya nakalamilioni mbili alizorekodi.
Manamo mwaka 1995 CD yake ya Shwele Baba aliuza zaidi ya nakala miliono moja baada ya muda wa wiki tatu, na kumfanya kuwa katika nafasi ya juu kwa uuzaji wa CD nchini Afrika ya kusini katika historia ya muziki. Mwaka 1996 aliondokewa na baba yake mzazi, kaka yake pamoja na dada yake ambapo alikuwa katika hali ya uzuni. Hicho hakikumfanya aache kuendelea na muziki, kutu alichoami kwamba hatma ya maisha yake iko mikononi mwa Mungu.
Tuzo alizoshinda ni tuzo ya mwimaji bora ‘Best Gospel Singer’ 1994, Tuzo ya muuzaji bora wa albamu ya ‘Uzube Nam’ 1997, Msanii bora wa nyimbo za injili Afrika na muuzaji bora wa albamu ya Angindedwa 1998, Msanii bora wa kike na ubora wa wimbo wa kiafrka wa Somlandela 1999, msanii bora wa wimbo wa Sabel Uyabizwa 2002,msanii bora wa kiafria wimbo wa Iyahamba Lenqolq 2003 na tuzo ya msanii bora wa kiafrika wimbo wa Hlala Nami 2004.
Nyimbo alizofanikiwa kurekodi ni kama vile Hola-Ma-G-Man 1998, Shwele Baba 1995, Uzube Nam 1996, Live at the State Theatre 1996, Angingedwa 1997, Free at last: South Africa Gospel 1997, Somlandela 1998, Ukholo Lwam 1999, Siyabonga 2000, Sabel Uyabizwa 2001, Ngiyekeleni 2002, Iyahamba Lengola 2002, Hlala Nami 2003.
Malkia huyu wa nyimbo za injili Afrika ya Kusini anatarajia kusimama jukwaa moja na mshindani wake Benjamini Dube, maonyesho hayo yakiwa yameandaliwa na kampuni ya Isambulo Music, inayoongozwa na Mhlonishwa Motsa, ambae ni raisi wa jumuiya ya wasanii wa kikristo Swaziland (ACASWA).
Pia muimbaji huyu amefanikiwa kutembelea mataifa tofauti tofauti, na nyimbo zake kupendwa na watu mbalimbali ulimwenguni.
Comments
Post a Comment