ROSE MUHANDO: Malkia wa muziki wa injili nchi Tanzania
Rose
mhando ni muimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania na afrika ya mashariki
kwa ujumla ambaye alianza kutambwa mwaka 2004 na albamu ya Uwe Macho ambayo
ilipendwa na watu wengisana.
Awali
muimbaji huyu kabla ya kuwa mkristo, alikuwa muumini wa dini ya kiislamu,
baadaye alipokuwa na umri wa miaka tisa anasema akiwa amelala alipata maono ya
Yesu Kristo.
Pia
anasema aliteseka kwa muda wa miaka mitatu na kuamua kubadilisha dini kwa
kupokea wokovu na kuwa mkristo, ambapo baadaye alianza kuimba muziki wa injili
kama mwalimu wa kwaya inayojulikana kama kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa
la Anglikana linalofahamika kama Chimuli lilipo mkoani Dodoma.
Tangu
aanze kuimba muziki wa injili amefani kiwa kutunukiwa tuzo tatu ambapo tuzo ya
kwanza alitunukiwa tuzo ya muimbaji bora wa kike na nyimbo za dini 2005 tuzo ya
Tanzania Music Award wimbo ukiwa “Mteule uwe macho”, 2009 alipata tuzo ya
Tanzania Gospel Singer Awards ya mwimbaji bora nchini Tanzania ambapo
alizawadiwa fedha za kitanzania sh. 200,000, vilevile 20o8 alipata tuzo ya
Kenya Groove Award ya muimbaji bora wa kike barani Afrika.
![]() |
Rose Muhando akiwa ameshika tuzo |
Rose
Muhando amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa Mkoani
Morogoro nchini Tanzania na ni mama wa watoto watatu, ambapo mpaka sasa
amefanikiwa kutoa kadhaa kamavile Uwe Macho 2004, kwaya ya Kitimtim jina la albamu Uinuliwe Baba2005, Jipange Sawasawa 2008, Utamu wa Yesu, na Pindo la yesu, kwa sasa anatamba
na wimbo wa Facebook.
Comments
Post a Comment