REBECCA MALOPE: Malkia wa muziki wa injili Afrika ya Kusini

Rebecca Malope amezaliwa mwaka 1968 karibu na Nelspruit mji mkuu wa Mpumalanga, Siku za nyuma alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu hivyo alishindwa kuendelea kusoma, kiufupi tu ni kwamba alipokuwa motto mdogo alikuwa akitumia baiskeli za walemavu kutembelea kutokana na kuumwa sana na kwa muda mrefu ambapo iliwapelekea hata madaktari kuamini kwamba hataweza kutembea tena. Malkia wa nyimbo za injili Afrika ya Kusini Rebecca Malope akiwa ameshika tuzo. Familia yake ilikuwa maskini sana, ambapo mnamo mwaka 1986 Rebeka pamoja na dada yake Cynthia walitembea umbali wa kilomita 400 kutoka nyumbani kwao kwenda Johannesburg mjini Evaton kutafuta kazi. Mnamo mwaka 1986 Rebecca aliingia kikundi cha kusaka vipaji kilichojulikana kama ‘Shell Road Fame’ lakini hakufanikiwa. Hakujali hilo akaingia tena mwaka uliofata na hatimae akashinda kuwa mwimbaji bora katika aina ya usololisti pamoja na Shine On . Tuzo aliyoipata baada ya kuwa mshindi iliwakilisha katika soko la muzi...