Ambwene Mwasongwe: Msanii anaekonga mioyo ya watu
Ambwene Mwasongwe ni msanii ambae
nyimbo zake zimebeba ujumbe murua, ambao
unawavutia watu wa aina mbalimbali walio wakristo na hatata watu wa dini
zingine kusikiliza.
Mwasongwe amekuwa na uimbaji wa
tofauti na wasanii wengine Afrika ya mashariki na barani Afrika , hasa katika
utunzi wa nyimbo zake ambazo zinakuwa zimebeba ujumbe mzito ambao mtu yeyote
akisikiliza zinamfanya atafakari zaidi.
![]() | |
Ambwene Mwasonwe akiwa anaimba. |
Moja kati ya nyimbo zake ambazo
watu wengi wamekuwa wakipenda kusikiliza ni MAJARIBU NI MTAJI, MISULI YA IMANI na
UPENDO WAKWELI hizi ni baadhi ya nyimbo za Mwasongwe ambazo
zinasikilizwa kwa kiasi kikubwa.
Msanii huyu amezaliwa mwaka 1985,
ambapo alianza kuimba nyimbo za injili akiwa na umri wa miaka 16 na kutoa
albamu yake ya kwanza inyoitwa Majaribu ni mtaji, akiwa na miaka 19, ikiwa
mpaka sasa ametoa albamu tatu yapili ikiitwa Heshima ya mrefu ni mfupi maarufu kama mzee
wa siku, na ya tatu ni Misuli ya imani.
Pia mwasongwe amekuwa akitamani sana nyimbo zake zifuke ulimwenguni kote, na sio Tanzania tu ili kuwatia moyo watu wanaopita kwenye mazingira tofauti tofauti na magumu ili wazidi kusonga mbele.
Nyimbo zake zinatubariki sana....tunakuombea kwa Mwenyez Mungu akubarik zaidi na zaid na akuweke ili tuzid kubarikiwa
ReplyDelete